Jeshi la Polisi nchini Tanzania limeendelea na msimamo wake wa kupinga wapigakura kukaa umbali wa mita 100 nje ya vituo vya kupigia kura kwa kile kinachosemwa na vyama vya upinzani kuwa ni "kulinda kura zisichakachuliwe" hapo tarehe 25 Oktoba, likisisitiza kuwa mkusanyiko wa aina hiyo unaweza kupelekea uvunjifu wa amani.