Polisi ya Ujerumani yaanzisha msako baada watu kuuwawa
20 Aprili 2025Matangazo
Kwa mujibu wa polisi ya jiji la Giessen miili ya wawili hao waliouawa, wote wakiwa na majeraha ya risasi, ilipatikana Jumamosi Alasiri katika eneo la makazi ya watu katika mji huo ulioko kilometa 25 kaskazini mwa Frankfurt, Taarifa ya polisi iliongeza kwa kusema kikosi kikubwa kuanzia wapelelezi, wa kawaida na matawi ya vikosi maalum wamejitokeza, wakisaidiwa na helikopta, kutafuta mhalifu au wahusika. Hata hivyo haijaweza kufahamika mara moja kiini cha mauaji hayo.Na polisi inaendelea na uchunguzi wake.