POLISI YA UBELGIJI
11 Machi 2005Matangazo
BRUSSELS:
Polisi ya Ubelgiji ilikomesha mapema leo asubuhi kukaliwa kwa ndege ya shirika la LUIFTHANSA.Msemaji wa Polisi aliarifu kuwa wote isipokuwa watatu kati ya walioikalia ndege hiyo 59 kulalamika walikataa kutoka ndani ya ndege hiyo kwa hiyari.
Polisi baadae ikaiparamia ndege hiyo na kuwakamata abiria waliosalia.
Abiria walioikalia ndege hiyo na kutotaka kutoka kwa muda wa masaa 13 walisemekana kuwa ni raia wa nchi za Ulaya.Ndege hiyo iliwasili Brussels kutoka Frankfurt.
Katika taarifa yao hapo kabla,kundi la abiria hao lilisema linautakla Umoja wa Ulaya kukomesha ushirikiano wote na serikali ya Iran na walidai kuzungumza na wabunge wa Ulaya.
.