Polisi Italia yakamata watuhumiwa 150 wa mtandao wa Mafia
11 Februari 2025Matangazo
Mahakama ilitoa waranti wa kukamatwa watu 183 ikiwemo 36 waliokuwa chini ya mikono ya polisi kwa tuhuma za kuendesha mtandao wa uhalifu, kujaribu kuua, kuwatesa watu, kusafirisha dawa za kulevya na kuchezesha kamari bila vibali. Waziri Mkuu wa Italia, Giorgia Meloni ameisifu operesheni hiyo inatajwa kuwa ndiyo kubwa zaidi kuwahi kulilenga kundi la mafia la Cosa Nostra tangu mwaka 1984. Ingawa nguvu za kundi hilo linaloundwa na koo za kisiwa chs Sicily zimepungua, polisi imesema uchunguzi wao wa miaka miwili umebaini kwamba bado linaratibu shughuli za uhalifu kupitia mawasiliano ya simu za siri.