Polisi wazima moto kwa kutumia barafu Urusi
23 Novemba 2018Matangazo
Kwa mujibu wa wizara ya mambo ya ndani ya Urusi, wakati polisi hao wakiwa katika doria katika eneo la Krasnojarsk, waligundua kwamba kuna moshi unatoka kutoka katika kibanda cha kuegeshea magari. Wakati moto huo ukikaribia kushika katika nyumba karibu na kibanda hicho, polisi hao walichukua barafu iliyotanda katika eneo hilo na kufinyanga kama mipira midogo na kushambulia moto huo hadi kuuzima. Polisi hao wawili wamepata medali ya ushujaa.