Polisi wauawa katika mashambulio Iraq:
15 Desemba 2003Matangazo
BAGHDAD: Hata baada ya kutiwa mbaroni mtawala wa zamani wa Iraq Saddam Hussein, linaendelea bado lile wimbi la mashambulio ya umwagaji damu. Watu si chini ya tisa wameuawa na wengine kadha kujeruhiwa viliposhambuliwa kwa mabomu vituo viwili vya polisi katika eneo la mji mkuu Baghdad. Watu wanane waliuawa bomu liliporipuliwa huko Husseiniyya, KM kama 30 Kaskazini mwa mji mkuu huo wa Iraq. Dereva wa gari aliuawa liliporipuka bomu katika gari yake kwenye kituo cha polisi katika mtaa wa Ameriyya mjini Baghdad. Ni hapo jana tu walipouawa watu 17 kiliposhambuliwa kituo cha polisi.