Uturuki: Polisi wamshikilia Ekrem Imamoglu, meya wa Istanbul
20 Machi 2025Imamoglu wa chama kikuu cha upinzani cha CHP ndiye mpinzani mkuu wa Rais Recep Tayyip Erdogan, na kukamatwa kwake kunajiri siku chache tu kabla ya chama hicho kutarajiwa kumtangaza kama mgombea wake katika uchaguzi wa rais wa mwaka 2028.
Imamoglu mwenye umri wa miaka 53 , amekuwa akilengwa na idadi inayoongezeka ya kile wakosoaji wanasema ni uchunguzi wa kisheria unaochochewa kisiasa. Maelfu ya watu waliandamana licha ya uwepo mkubwa wa polisi. Gavana wa Istanbul amepiga marufuku maandamano yote kwa muda wa siku nne.
Mameya kutoka miji mikuu kadhaa ya Ulaya ikiwa ni pamoja na Amsterdam, Paris, Milan, Barcelona, Rome, Helsinki, Gent (Ubelgiji), Utrecht na Brussels, wamelaani vikali kukamatwa kwa Ekrem Imamoglu na kutoa wito wa kuachiliwa kwake.