Sheria na HakiAfrika
Sudan: Polisi yaishutumu RSF kwa mauaji ya watu 11
17 Machi 2025Matangazo
Polisi ilisema jana kuwa miili 11, ikiwemo ya wanawake na watoto, iligundulika Jumamosi ndani ya kisima kirefu kwenye kitongoji cha Fayhaa.
Kanali Abdul-Rahanan Mohamed Hassan, mkuu wa kikosi cha raia mjini Khartoum, amesema msako katika eneo hilo ulianzishwa baada ya wakaazi kuripoti kwamba waliikuta maiti moja ndani ya kisima.
Soma pia:Sudan, Somaliland zakataa kuhusika na mpango wa kuwapokea Wapalestina kutoka Gaza
Polisi wamesema watu hao waliuawa na vikosi vya RSF, kabla ya kutupwa kwenye kisima, wakati wanamgambo hao walipokuwa wakilidhibiti eneo hilo.