PKK yatangaza kuweka chini silaha
12 Mei 2025Matangazo
Chama cha Wanamgambo wa Wakurdi nchini Uturuki cha PKK kimetangaza rasmi kuwa tayari kuweka chini silaha na kujivunja kama sehemu ya juhudi mpya ya amani na serikali ya Uturuki, kumaliza mgogoro wa kivita wa miongo minne.
Uamuzi wa PKK, umetangazwa na shirika la habari la Firat, baada ya kufanyika kongamano kubwa la chama hicho Kaskazini mwa Iraq.Soma pia:Wito wa Ocalan wa kukivunja chama chake cha PKK wapongezwa
PKK limeahidi kumaliza moja ya uasi wa muda mrefu zaidi katika kanda ya Mashariki ya kati na hatua hiyo huenda ikawa muhimu nchini Uturuki,Syria na Iraq.
Mwezi Februari kiongozi mkuu wa kundi hilo Abdullah Ocalan aliyeko jela tangu 1999 mjini Istanbul alilitaka kundi hilo kuitisha kongamano na kutangaza rasmi uamuzi wa kulivunja.