Pistorius akataa Ujerumani kubadili sera kuelekea Urusi
13 Juni 2025Waziri huyo wa ulinzi amesema kuwa mashambulizi ya hivi karibuni ya Moscow dhidi ya raia nchini Ukraine yanathibitisha kwamba haujafika muda wa kubadilisha mtazamo wa Berlin kuelekea Kremlin.
Pistorius, ambaye ni mmoja kati ya viongozi wenye ushawishi ndani ya SPD, ambacho ni mshirika mdogo kwenye serikali ya mseto ya Ujerumani, amesema haiwezekani mtu kuwa na fikra ya kusaka ushirikiano wa karibu na Urusi katika wakati kama huu.
Soma zaidi: Ujerumani yaahidi msaada zaidi kwa Ukraine
Kauli ya waziri huyo wa ulinzi wa Ujerumani imetolewa kufuatia hoja ya watu mashuhuri ndani ya chama chake inayotaka Ujerumani ibadili muelekeo wake kuhusu Urusi.
Manifesto iliyosainiwa na kiongozi wa zamani wa wabunge wa SPD, Rolf Mützenich, kiongozi wa zamani wa chama hicho, Nobert Walter-Borjans, mtaalamu wa sera za nje, Ralf Stegner, pamoja na wajumbe kadhaa wa mabunge ya majimbo na bunge la taifa, inataka kuwepo mazungumzo ya moja kwa moja na Moscow na kukosowa mipango ya serikali kuipa tena silaha Ukraine.
Akimnukuu kansela wa zamani wa Ujerumani kupitia SPD, Willy Brandt, Pistorius amesema muasisi huyo aliunga mkono Ujerumani kuwa na uwezo mkubwa wa kijeshi, kwa sababu alijuwa kuwa majadiliano na Wasovieti yanaweza tu kufanyika ikiwa Ujerumani ni imara.
Urusi yaimarisha kikosi chake cha droni
Ujerumani ni ya pili kwa utoaji silaha kwa Ukraine baada ya Marekani, na ziara ya Pistorius mjini Kiev inatajwa kuangazia uwezekano wa kuendelea na jukumu hilo, hasa katika wakati ambapo Marekani inaonekana kuelemea zaidi kwenye kusaka muafaka badala ya kuendeleza msaada ya kijeshi.
Hayo yanajiri wakati Rais Vladimir Putin wa Urusi akisema kwamba droni zimekuwa na jukumu kubwa kwenye vita vya nchi yake dhidi ya Ukraine na ametowa wito wa kuundwa haraka kwa vikosi maalum vya ndege hizo zisizo rubani kwenye jeshi.
Soma zaidi: Kundi la "Ramstein" laapa kuendelea kuisaidia Ukraine kijeshi katikati ya vita na Ukraine
Akizungumza kwenye siku ya pili ya mkutano wa masuala ya kijeshi mjini Moscow, Putin amesema kwa sasa nchi yake inaunda mifumo ya isiyolazimika kuwa na wa