Makala ya Utamaduni na sanaa inamuagazia kwa undani Philo Tsoungui, mmoja wa wapigangoma maarufu zaidi wa kike nchini Ujerumani. Akitokea katika familia mchanganyiko, mama Mjerumani na Baba kutoka Kameruni, Philo, sio tu anapambana kuvuka vizuizi vya mfumo dume, bali pia changamoto za ubaguzi dhidi ya watu weusi.