Paul Pogba akamilisha kutumikia kifungo
11 Machi 2025Marufuku ya Paul Pogba kutocheza soka kutokana na kesi yake ya kutumia dawa za kutunisha misuli inafika mwisho leo Machi 11.
Kwa mujibu wa Kiungo huyo wa zamani wa klabu ya Juventus ana fursa kadhaa za kuanza upya taaluma yake, ikiwemo kuichezea timu ya Inter Miami na Al-Shahad ya Pavel Nedved.
Kiungo wa Ufaransa Pogba yuko tayari kurejea uwanjani kusakata kandanda siku 569 tangu alipofeli vipimo vya dawa za kusisimua misuli huko Udinese, Juventus.
Kiungo huyo wa zamani wa klabu ya Juventus na Manchester United alipigwa marufuku asicheze soka kwa miaka minne, lakini hukumu hiyo baadaye ikapunguzwa hadi miezi 18. Kwa maana hiyo, Pogba yuko sokoni kama wakala huru kuanzia Machi 11, 2025 na anaweza kucheza katika ligi yoyote kati ya tano bora za Ulaya, ikiwemo Bundesliga. Kufikia sasa hakujawa na taarifa zozote kuhusu klabu ya Bundesliga inayohitaji huduma zake.
Soma pia: Dawa za kusisimua misuli: Paul Pogba asimamishwa kwa muda
Pogba anatafakari uwezekano wa kuendelea kusakata soka la kulipwa, akiangazia hasa ligi kubwa za Ulaya. Amehusishwa na klabu ya Marseille na Manchester United.
Mnamo Februari 29, 2024, Pogba alipigwa marufuku kwa miaka minne kwa kukiuka sheria za udhibiti wa dawa za kutunisha misuli, kifungo hicho kikianza kutekelezwa Septemba 11, 2023. Baadaye mahakama ya usuluhishi wa kesi za michezo, CAS, iliipunguza marufuku hiyo hadi miezi 18.