PARIS:Viongozi wa Umoja wa Ulaya wasikitishwa na uamuzi wa wafaransa
30 Mei 2005Viongozi wa Umoja wa Ulaya wametoa sauti zao kwa haraka juu ya kupingwa kwa katiba mpya ya Umoja huo na wananchi wa Ufaransa katika kura ya maoni ya hapo jana.
Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Jack Straw akizungumza na wandishi habari kuhusu suala hilo alisema matokeo hayo yanahitaji muda wa kufikiriwa tena kwa ajili ya hatma ya baadaye ya Umoja huo.
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani naye upande wake alisema Uamuzi uliochukuliwa na wafaransa ni wa kusikitisha na umeiweka ulaya katika changamoto kubwa.
Rais wa tume ya Umoja huo bwana Jose Manuel Barosso ameutaja uamuzi huo kuwa tatizo linalohitaji kutatuliwa.
Huku Kansela wa Ujerumani Gerhard Scroeder akisema kwamba kukataliwa kwa katiba hiyo mpya ya Umoja wa Ulaya na Wafaransa ni pigo kubwa lakini haimanishi mwisho wa Katiba hiyo.