PARIS:Umoja wa Ulaya wasitisha mazungumzo na Iran
24 Agosti 2005Matangazo
Wizara ya mambo ya nchi za nje ya Ufaransa imeeleza kwamba jumuiya ya Ulaya imefutilia mbali mazungumnzo yaliyokuwa yafanyike Agosti 31 juu ya suala la mpango wa Nuklia wa Iran.
Mkutano huo ulikuwa na lengo la kuishawishi Iran iachane na shughuli zake za Kinuklia.
Msemaji wa wizara hiyo Jean Baptiste Mattei amesema mazungumzo hayo yamefutiliwa mbali kwa sasa kufuatia hatua ya Iran ya kuanzisha tena shughuli zake za kurutubisha madini ya Uranium na kukiuka ahadi ya kusiamamisha shughuli hizo ili mazungumzo yaendelee.
Umoja wa Ulaya pamoja na Marekani zinashuku kuwa Iran inatengeneza silaha za Nuklia kisirisiri lakini hata hiyvo Iran inashikilia kusema mpango wake ni kwa ajili ya nguvu za Nishati.