PARIS:Rais Jacque Chiraque asema suala la Iran liendelezwe kidiplomasia
19 Septemba 2006Rais wa Ufaransa Jacque Chirac amezitolea mwito nchi zenye nguvu duniani kuendelea na mazungumzo na taifa la Iran juu ya mpango wake wa Kinuklia.
Iran imepuuza muda wa mwisho uliokuwa umewekwa na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wa kuitaka nchi hiyo kusimamisha shughuli zake za kurutubisha madini ya Uranium ifikiapo Agosti 31 la sivyo ikabiliwe na vikwazo.
Licha ya Marekani kumpa Visa mpatanishi mkuu wa Iran katika mazungumzo ya Nuklia bwana Ali Larijani ili aweze kufika New-York wiki hii,Balozi wa Marekani katika Umoja wa mataifa John Bolton amekiri kwamba Larijani hajawasili na kwamba majadiliano na Iran yanaonyesha kama yamekwama.
Rais wa Iran Mahmoud Ahmed Nejad leo usiku anatarajiwa kulihutubia baraza la Umoja wa mataifa juu ya suala hilo la Nuklia.