PARIS: Waandamanaji wa kigeni kurudishwa nchini kwao
10 Novemba 2005Matangazo
Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy, ametoa amri ya kuwarudisha nyumbani waandamanaji wa kigeni watakaopatikana na hatia. Sarkozy ameliambia bunge mjini Paris kwamba watu 120 ambao wamepatikana na hatia ni raia wa kigeni na watarudishwa makwao hata licha ya kuwa na kibali cha kuishi nchini Ufaransa.
Uamuzi huu unafuatia hatua ya serikali kutangaza hali ya hatari, inayowaruhusu viongozi wa maeneo yaliyoathiriwa na machafuko kutangaza misako na kuwaongezea mamlaka polisi kuwasaka washukiwa na kuwakamata.
Magari kadhaa yamechomwa moto katika ghasia za usiku wa kuamkia leo lakini polisi wanasema machafuko hayo yamepungua nchini kote.