PARIS: Polisi wajeruhiwa katika machafuko mjini Paris
7 Novemba 2005Matangazo
Polisi zaidi ya 10 wamejeruhiwa mjini Paris Ufaransa katika machafuko yaliyoendelea kwa usiku wa kumi na moja mfululizo. Maofisa wawili wamepata majeraha mabaya wakati waandamanaji walipowafyatulia risasi.
Huku machafuko hayo yakiendelea katika sehemu mbalimbali za nchi hiyo, kutoka bahari ya Mediterenia hadi eneo la mpakani na Ujerumani, polisi wamesema bado hawajakabiliana na aina hiyo ya vurugu tangu kumaliza kwa vita vya pili vya dunia.
Duru za polisi zinasema vijana takriban 200 wametiwa mbaroni na motokaa zaidi ya 800 zimechomwa moto pamoja na majengo ya serikali na makanisa.
Rais Jacques Chirac amefanya mkutano wa dharura na maofisa wa serikali yake katika juhudi za kurejesha utulivu mjini humo.