PARIS: Hakuna maafikiano kuhusu mradi wa kinuklia wa Iran
25 Machi 2005Mkutano kati ya Iran na nchi tatu kuu za Umoja wa Ulaya umemalizika mjini Paris bila ya kukubaliana njia ya kuutenzua mgogoro unaohusika na mradi wa kinuklia wa Iran.Ujerumani,Ufaransa na Uingereza zinajaribu kuishawishi Iran isitishe mipango yake ya kuimarisha madini ya Uranium.Pindi itafanya hivyo basi Iran itapewa vichocheo vya kiuchumi,kisiasa na teknolojia.Uranium iliyo imarishwa inaweza kutumiwa kutengeneza silaha za kinuklia.Mjumbe mkuu wa Iran katika mazungumzo ya mjini Paris aliwaambia waandishi habari kuwa majadiliano zaidi yatafanywa katika kipindi cha wiki chache zijazo.Washington imeituhumu Teheran kuwa inajaribu kutengeneza silaha za kinuklia,lakini Iran inasema,miradi yake ya kinuklia inahusika na uzalishaji wa nishati ya umeme.