JamiiItaly
Papa Leo XIV awahimiza vijana kujenga dunia ya haki na amani
3 Agosti 2025Matangazo
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Leo wa XIV ametoa mwito huo wakati wa misa ya kufunga mkutano wa wiki nzima uliohusisha vijana wa kizazi kijacho cha Wakatoliki.
Mkutano huo ni tukio la kipekee linalofanyika kati ya Julai 28 hadi Agosti 3, likiwa sehemu ya Mwaka Mtakatifu wa Kanisa Katoliki na wenye la kuimarisha imani na mshikamano wa vijana wa kizazi kijacho kutoka duniani kote.
Inaripotiwa kwamba vijana kutoka mataifa 150 ikiwemo maeneo yenye migogoro kama vile Lebanon, Iraq, Ukraine, Syria na Sudan Kusini pia walihudhuria.
Vatican imesema zaidi ya vijana milioni moja walihudhuria, wakiwemo pia mapadre 7,000 na maaskofu 450