SiasaMamlaka ya Palestina
Papa Leo XIV asistiza umuhimu wa kulinda maeneo ya ibada
18 Julai 2025Matangazo
Hatua hii inajiri baada ya shambulio laIsrael kwenye kanisa pekee la Kikatoliki katika mji wa Gaza.
Papa Leo alirudia wito wake wa kufanyika mazungumzo, kusitisha mapigano, na kumaliza vita, huku akielezea tena wasiwasi wake kuhusu "hali mbaya ya kibinadamu" katika ardhi za Palestina.
Vatican imethibitisha kuwa Netanyahu ndiye aliyeanzisha mazungumzo hayo kwa njia ya simu, siku moja baada ya shambulio la kijeshi lililowaua watu watatu katika Kanisa la Holy Family.
Papa Leo XIV ameeleza kuwa mashambulio dhidi ya maeneo ya kidini yanahatarisha misingi ya utu na amani.