Papa Leo wa XIV atowa mwito wa amani duniani
11 Mei 2025Maelfu ya waumini wa kanisa Katoliki wamemiminika Vatican, mjini Rome kushiriki misa ya Jumapili, ambako papa Leo XIV ameongoza kwa mara ya kwanza sala ya baraka ya Jumapili tangu alipochaguliwa kuliongoza kanisa hilo duniani.
Soma pia:Viongozi wa ulimwengu wampongeza kiongozi mpya wa kanisa katoliki Papa Leo XIVMiongoni mwa mambo aliyoyatanguliza kwenye hotuba yake, ametowa mwito wa kufikiwa amani ya kweli na ya haki itakayodumu nchini Ukraine huku akisisitiza juu ya kusitishwa vita katika Ukanda wa Gaza pamoja na kuachiwa huru kwa mateka wanaoshikiliwa na kundi la Hamas.
Kadhalika amewahimiza viongozi wa dunia kutounga mkono kabisa vita duniani akisema umefika wakati wa kuachana na migogoro.
Misa hiyo ya baraka ya Jumapili hutolewa kutokea kwenye dirisha linalotazama uwanja wa kanisa kuu la mtakatifu Petro lakini papa Leo wa 14 atatowa baraka za Jumapili, tangu alipochaguliwa siku tatu zilizopita kupitia roshani alikosimama wakati akitangazwa kuwa Papa.
Misa ya baraka ya Jumapili ni ibada muhimu kwa Wakatoliki ikiwa pia ni fursa ya kipekee kwa waumini wa kawaida ya kumuona Papa kwa ukaribu zaidi.
Soma pia:Kanisa Katoliki: Papa Leo XIV atangaza sera za uongozi wakePapa Leo XIV , siku ya Jumamosi aliwahutubia makadinali ambapo alijishusha mbele ya kanisa akisema yeye ni mtumishi myenyekevu wa Mungu na hakuna zaidi ya hivyo na pia ni mrithi asiyekuwa na ''thamani'' yoyote wa mtakatifu Petro.