Papa Leo azitaka Iran na Israel kuwajibika na matendo yake
14 Juni 2025Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Leo XIV ametoa wito kwa Israel na Iran kuonyesha hali ya uwajibikaji katika matendo yao wakati mzozo kati ya mahasimu hao wawili ukizidi kufukuta.
Katika taarifa yake aliyoitoa leo Jumamosi, Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki, amesema hali nchini Iran na Israel imezorota sana katika wakati ulio mgumu.
Papa Leo ameongeza kuwa jukumu la kujenga dunia iliyo salama isiyo na kitisho cha nyuklia ni lazima lifanyike kwa njia ya mikutano na mazungumzo, na kwamba hakuna mtu anapaswa kutishia uwepo wa mwingine.
Israel imesema kuwa mashambulizi yake dhidi ya Iran siku ya Ijumaa, yalifanywa ili kuizuia nchi hiyo kuendeleza silaha za nyuklia.
Wakosoaji wanasema mashambulizi hayo ya Israel kimsingi yalikuwa batili chini ya sheria za kimataifa.