Papa Francis aonekana hadharani kwa mara ya kwanza Jumapili
23 Machi 2025Matangazo
Papa Francis mwenye umri wa miaka 88 anapanga kutoa baraka za Jumapili kutoka kwenye chumba maalum katika ghorofa ya 10 katika hospitali ya Gemelli ya mjini Roma.
Baadaye Papa Francis atawaaga wafanyakazi wa hospitali hiyo na kurejea Vatican ambako atapumzika kwa angalau miezi miwili. Madaktari wanamshauri kujizuia kukutana na makundi makubwa ya watu au kufanya shughuli za kujichokesha.
Taarifa hizi zinatoa matumaini kwa wakatoliki na watu wengine duniani kote ambao wamekuwa wakimuombea Papa Francis apone haraka.
Hadi sasa bado haijajulikana iwapo ataweza kuongoza ratiba za matukio muhimu ya kidini hasa kuelekea Pasaka kufuatia kulazwa kwa muda mrefu.